GET /api/v0.1/hansard/entries/1014420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1014420,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014420/?format=api",
    "text_counter": 311,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nami nichangie. Mwanzo, ningependa, moja kwa moja, niunge mkono Kamati. Tunapouliza maswali ama tunapoleta petitions, huwa kuna sababu za kutufanya tufanye hivyo. Baada ya kuleta maombi haya, ikiwa hakuna linalofanyika, basi huwa zile sababu zetu hazijapata suluhisho. Kwa hivyo, ni muhimu tunapouliza maswali, yanapojibiwa, yawe yenye kufuatiliwa ili shida zilizoko mashinani ziweze kutatuliwa ama huduma kwa mwananchi iweze kupatikana. Pia, ingawaje wakati mwingine shughuli hiyo hufanyika, huwa inachukua muda kufanyika. Wakati mwingine inapofanyika, inakuwa imepitwa na wakati. Kwa mfano, tunapouliza Swali, tuseme msimu wa matikiti maji, kabla swali hilo lishughulikiwe, ule msimu umeisha kabisa! Sasa ni kama lile swali ulilouliza halikuwa na maana. Sitaki kuchukua muda mwingi kwa sababu nilisikia kuwa ni watu watatu wanaostahili kuzungumza ili tumpe nafasi Mwasilishi Hoja aendelee. Sitaki kuchukua muda mwingi. Wacha nikomee hapa ili tupate kuendelea. Ahsante."
}