GET /api/v0.1/hansard/entries/1014528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1014528,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014528/?format=api",
    "text_counter": 46,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati. Kwanza, ningependa kusema kwamba sisi kama Maseneta ni Waheshimiwa na lazima tuendeshe mambo yetu tukiwa na heshima. Aidha tukiwa katika Bunge ama hata tukiwa nje ya Bunge, lazima maadili yetu tuyafuate kama Waheshimiwa. Pili ni kuwa ni jambo la kupendeza kwamba hawa Maseneta wawili, Sen. Kwamboka na Sen. Seneta, wameweza kuomba msamaha na wakajutia makosa yao. Kwa hivyo, ni sisi kama Bunge kukubali Ripoti ya Kamati ili waweze kusamehewa na warudi kwa miungano yao kama kawaida. Tumechaguliwa kuhudumu kwa miaka mitano. Kwa hivyo, ikiwa tutaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, ina maana kwamba itakuwa vigumu kutekeleza malengo na shabaha ya Bunge. Kwa vile wameweza kukubali kwamba walikiuka maadili kwa upande fulani, ni jambo la sawa kwamba waombe msamaha ili tuweze kusonga mbele. Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii."
}