GET /api/v0.1/hansard/entries/1014947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1014947,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014947/?format=api",
    "text_counter": 465,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii fursa ya kuchangia hii Ripoti ya MES. Huu mradi ulikuwa mzuri sana ambao ulisaidia kaunti kupata vifaa na kuhakikisha kwamba vituo vya afya vinapata vifaa vya kuboresha huduma. Bw. Spika, huu mradi haukuwa na mpangilio wa kutosha kuhakikisha kwamba unafaulu. Kwa mfano, tumeambiwa na Ripoti ya kwamba kuna hospitali zilizopelekewa vifaa, lakini hakukuwa na miundo msingi ya kutosha kuhakikisha ya kwamba hivi vifaa vinafanya kazi. Kwa mfano, kuna vituo vya afya ambavyo havikuwa na maji ama umeme. Kama huu mradi ungekuwa umepangiwa vizuri ili kufaulu, kungekuwa na mipangilio madhubuti ya kuweka umeme ama maji. Bw. Spika, kuna watu wa kulaumu kama vile magavana. Kwa mfano, itakuwaje kifaa cha huduma za afya kisifanye kazi kwa sababu hakuna umeme? Ni kazi ya nani kuweka umeme kwa vituo vya afya? Ni kazi ya gavana ama serikali za uagatuzi. Katika kuweka lawama ama dhambi hii, lazima pia magavana pia wapate lawama yao. Hii ni kwa sababu ni pesa za magatuzi zilizopelekwa huko, zilikatwa na vifaa vimekuja lakini havikuweza kutumika. Bw. Spika, kuna baadhi ya Maseneta ambao wamesema kwamba tulikuwa na lawama kidogo kwa sababu tulipitisha pesa ziende kwa kutafuta vifaa vya afya, na hatukuangalia hizo bei ama kandarasi ambayo zilikuwa zinapitiswa. Huu mradi unahitajika hata siku za usoni. Kwa hivyo, inatakikana pia tushikane na Serikali ama Idara ya Afya kuangali ni vipi wakati hiyo miaka saba ya hii lease ya MES The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}