GET /api/v0.1/hansard/entries/1014968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1014968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014968/?format=api",
    "text_counter": 486,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Tumeelezwa kwamba mradi wa MES ulikuwa utumike kwa muda wa miaka saba. Miaka mitatu imekwisha na bado hakuna vifaa vingine vipya. Hivi vifaa vilikua vimekodishwa kaunti zetu. Baada ya miaka saba, je, vifaa hivi vitarudi kwa waliokodisha ama vitanunuliwa na kaunti zetu ili watu wetu waendelee kupata huduma? Kwa kumalizia, Kamati imesema kwamba kuna makosa fulani ambayo yalifanyika kisheria, lakini hatukuweza kuona hata mmoja ambaye amenyoshewa kidole kusema ya kwamba wewe umefanya makosa haya. Hii Ripoti kama alivyotangulia kusema Mhe. Mwaura, ni kwamba, ni kama kupiga domo kaya; hakuna mwelekeo wowote ambao sisi tunaweza kuchukua kama Seneti kuhakikisha ya kwamba wale ambao walifuja pesa za umma na kufanya makosa kadhaa, wameletwa mbele ya korit ili waweze kushtakiwa."
}