GET /api/v0.1/hansard/entries/1015000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015000/?format=api",
"text_counter": 518,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Huu mradi ulipoingia, watu wengi sana waliufurahikia. Mimi kama Seneta, niliufurahia ulipoingia katika nchi yetu. Hii ni kwa sababu watu wengi walipata huduma. Ingawa kuna ripoti zingine za wananchi wanasema kwamba, pesa zimefujwa, hii ni kawaida. Waswahili wana msemo wao wanasema: “Hata ukifanya vyema katika nchi hii, lazima utaongelewa.” Kwa hivyo, ninaunga mkono Kamati hii kwa kazi waliyofanya. Ripoti yao imefanywa vizuri sana. Walizunguka katika Kaunti ya Mombasa, wakaenda Tana River na kaunti zingine vile tulivyowaona katika runinga. Kwa hivyo, ninishukuru sana Kamati hii na Mwenyezi Mungu awajalie kwa kazi waliofanya. Asante."
}