GET /api/v0.1/hansard/entries/1015392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015392,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015392/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "o",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Vile nilivyotangulia kusema, ningetamani sana nione ile nguvu wenzetu wa Seneti waliitumia kwa kujadili Kshs316 bilioni na vile zitagawanywa katika kaunti zetu. Wangetumia nguvu hizo kupigana na ufisadi ambao unaendelea katika magatuzi yetu. Walitumia nguvu nyingi sana lakini wenzangu wengi wameongea kwamba wakati mwingi, kuna ufujaji wa pesa sana katika magatuzi yetu. Wenzetu wa Seneti hawajatumia nguvu ile kuangalia na kutilia maanani kwamba pesa zinazoenda kwa magatuzi zimetumika vyema."
}