GET /api/v0.1/hansard/entries/1015393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015393/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "o",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Kwa haraka tu, ningependa kusema hivi. CRA ambayo imeleta formula hii ambayo ilipelekwa kwa Seneti na leo hii Seneti wakajadili ikaja kwetu imeongea juu ya mambo ya kilimo. Hizi takwimu za mambo ya kilimo zinasukuma nje sana serikali gatuzi ambazo hazijabobea kwa mambo ya kilimo. Kama vile wenzangu wamesema, kuna serikali gatuzi ambazo zinategemea uvuvi wa samaki. Kuna serikali gatuzi pia kama Taita Taveta kule nitokako, ambako hatuwezi kilimo kwa sababu ya shida tulizonazo dhidi ya wananchi na wanyama wa pori. Wakati wanaweka takwimu ya juu kwa mambo ya kilimo, sisi ambao hatuwezi kufanya kilimo kwa sababu ya shida hizi za wanyama wa pori, inatudhulumu. Pili, sisi ambao tunakaa mahali ambapo maji haijatajwa katika takwimu hii tunaumia. Sababu ya kutokuwa na maji ndio inafanya wengine wetu ama wale The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}