GET /api/v0.1/hansard/entries/1015394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015394,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015394/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "o",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "tunatoka kwa kimombo ASAL tunashindwa kufanya kilimo ama maendeleo mengine. Kwa hivyo, Seneti na CRA ingetilia mkazo mambo ya maji kuliko kilimo. La mwisho ni mambo ya afya. Wengine wetu tunajua kwamba kuna zahanati za afya ambazo zimebobea sana katika serikali gatuzi nyingi. Kuna serikali gatuzi ambazo ningetaka kusema, kama mahali Mhe. Shaban anatoka, wananchi wengi hawaendi hospitalini kwa sababu hazina vifaa, madawa na miundo msingi mhimu ya kusaidia watu wetu. Inabidi wavuke waende nchi jirani. Wakisema idadi ya watu wanaotembelea zahanati, watu wengi ambao wanatoka nchini kwenda nchi jirani hawachukuliwi maanani. Tunapoteza idadi ya watu ambao wanatembelea zahanati kule nyanjani. Watu wengi hawaendi hospitali zetu. Kwa hivyo, fomula hii iliyotumika inadhalilisha maeneo ambayo yamebaki nyuma miaka nenda, miaka rudi. Kama tunaunga mkono, ni vizuri ziende katika kumbukumbu za Bunge kuwa CRA ikishirikiana na Bunge la Seneti, ni muhumi wachangamkie takwimu walizozitumia. Nyingi kati yazo si takwimu ambazo zina uhakika. Mfano ni wakati CRA ilileta fomula ya mambo ya kutengwa. Walitumia takwimu ambazo nilipinga na nikaketi na Commissioners wa CRA na wakaona takwimu hizo walizotumia si nzuri ama hazikua sawa. Waliweka maeneo mengine kuwa yalikua yamebobea. Ilibidi watembee kudhibitisha kuwa hawakutumia takwimu sawa. Naunga mkono, lakini nitasema ni vizuri tuchunguze kwa undani takwimu zinazotumiwa kwa sababu tukiendelea hivi, nchi yetu itabaki kuwa kwingine kutaendelea na kwingine kunabaki nyuma. Najua saa zimeisha lakini kuna pesa nyingi ambazo zinabaki katika Serikali kuu. Ni vyema kama Bunge la Kitaifa tunapojadili Bajeti ama Bajeti-nyongeza itakapoletwa, iletwe hesabu ya kweli kuonyesha pesa zinazobaki katika serikali za kitaifa zinatumika vipi. Kuna miradi mingi katika maeneo fulani na maeneo mengine yanabaki kuwa maskini. Naunga mkono. Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda."
}