GET /api/v0.1/hansard/entries/1015535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1015535,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015535/?format=api",
    "text_counter": 60,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika. Hili jambo kuhusiana na maswala ya miraa ni jambo ambalo ni tetesi, lakini nataka kukubaliana na mwenzangu, Mhe (Dr.) Pukose alivyozungumza kuwa, twawaomba na twawasihi ndugu zetu wale watakuwa wanatengeza hii ripoti, waangalie na athari zake. Upande moja ni kweli wenzetu wanaitegemea kwani ni kitegemeo cha uchumi, lakini kwingine, yafaa mkumbuke kwamba vijana chipukizi wanapoteza maisha yao kwa sababu ya haya mambo. Hususan siku hizi unapata muguka kipakti kimoja hivi kinakupeleka mbio na ni shilingi ishirini peke yake. Shilingi ishirini inakupeleka mbio ukajionakuwa wewe ni multi-millionaire na tunawasihi wanakamati, hii Kenya ni yetu sote. Ikiwa mnaangalia upande moja na upande mwingine hauangaliwi, itakuwa vibaya. Lazima tujue kuna athari hii na ni njia ipi tutahakikisha kuwa athari ile isiweze kufika katika maeneo mengine ya Kenya. Ahsante Mhe. Spika."
}