GET /api/v0.1/hansard/entries/1015632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015632,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015632/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Reli (Kenya Railways Corporation), na Shirika la kusafirisha mafuta (Kenya Pipeline) chini ya usimamizi wa shirika jingine la Industrial and Commercial Development Corporation (ICDC). Ningependa kuzungumzia Amri Kuu ya Rais ya tarehe 7 Agosti 2020 kuhusu mpangilio huu. Inasemekana kuwa muungano huo ni wa utendakazi peke yake wa mashirika husika. Tatizo ni kuwa Wakenya hawajahusishwa na mambo hayajawekwa wazi. Kwa hivyo, tunaomba tujulishwa kupitia Bunge hili ikiwa hili jambo ni kuunganisha ama ni jambo gani ambalo lilifanywa. Ikiwa ni masuala ya kuunganisha, basi wananchi walihusishwa kwa njia ipi kupitia yale matakwa ya Katiba, halmaarufu “ public participation ”? Najua umenipa dakika tatu. Jana, Kamati husika ya Uchukuzi ilileta ripoti kuhusiana na masuala ya Standard Gauge Railway (SGR). Ripoti hii ni ile tulizungumzia. Nimeisoma tayari. Ningeomba Kamati iharakishe ili tuweze kuimaliza na liwe jambo la kisawasawa. Pengine tuwaombe wale ambao hudandiadandia kule nje katika vibaraza waje hapa ambapo kanuni zinatengenezwa. Tuwafunze kuwa badala ya kuzungumzazungumza huko nje kuhusu mambo ya SGR, tuwaonyeshe njia ambayo sheria zinatengenezwa. Ni kazi ngumu lakini hayo ndiyo majukumu Wakenya walitupa. Tunashukuru tumefika kikomo lakini sasa tunaomba upeane nafasi ya haraka ili tuizungumzie Ripoti. Waswahili wanasema “mbuzi jamvi ashalila, Hasidi hatujui atakaa wapi sasa.”"
}