GET /api/v0.1/hansard/entries/1015744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1015744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015744/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ningependa kusema kuwa kijana huyu ambaye ni mlemavu, Mhe. Rais alimchagua kwa nia safi. Isipokua ukiangalia sheria vile ilivyo ni kuwa hakutoshea na hakubobea kuwa kwenye nafasi hiyo. Kuna umuhimu kuwa kijana huanza kwa kutambaa ndio aweze kukimbia. Mimi ningependelea kama walemavu na jamii ndogo kama Wakuria pia wangepatiwa nafasi. Hii ni kwa sababu ni haki yao kupatiwa nafasi. Lakini isiwe mtu anapewa kazi kama hajafanya kazi kwa muda unaofaa ama mrefu. Pia, kwa umri wake, kazi kama hii ni nzito si nyepesi. Nakubaliana na taarifa hii iliyotolewa na kamati hii kuwa hawa watatu wapatiwe kazi na huyu mmoja anzishwe kutambaa kwanza kabla hajafika kwenye kazi ya afisi kubwa kama hii."
}