GET /api/v0.1/hansard/entries/1015761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015761,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015761/?format=api",
"text_counter": 286,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": " Mhe. Spika, asante sana. Naunga mkono mjadala huu ambao ni muhimu sana. Pili, unapomsikia Mhe. Naomi Shaban akizungumza Kiswahili na akikiboronga sawasawa, unapata uchu kidogo nawe pia ukizungumze Kiswahili. Nimemuona ni mkiritimba na mtu ambaye ana ujuzi mwingi sana na ubabe katika lugha hiyo. Mimi kama Mjumbe wa Shinyalu, nasimama hapa kumuunga mkono Bi. Ann Nderitu. Ni afisa ambaye ninavyomjua, ana ujuzi mzuri na pia ana mahusiano mazuri na watu. Vilevile ana hulka na tabia nzuri. Tunaona kwamba anafaa sana kushikilia wadhifa huo katika kuendeleza gurudumu hili ambalo ni telezi. Kama mnavyojua, mara nyingi tumewajua wale waliokuwa pale mbeleni. Kuna Lucy Ndung’u ambaye pia alifanya kazi nzuri lakini ujue ukiwa kaimu, inakuwa vigumu sana wewe kutekeleza na kushikilia vizuri kwa sababu hujui kesho au siku utakayotolewa. Ningependa kumshukuru Rais kwa kumchagua yule mtu anafaa zaidi na pia kuzingatia majadiliano yaliyofanywa na shirika la kuajiri. Hiyo ni heko kwake. Ningependa kumwambia Nderitu akae ange kwa sababu inafika wakati ambapo tutakuwa na mambo mengi ya kudafilisha na kuchanganyachanganya. Kama mnavyojua, kuweka shajara mara nyingi huwa kuna mushikili kidogo. Unaweza kujikuta umo kwenye chama kingine ambacho si chako. Nakumbuka wakati nikitafuta uchaguzi wangu hasa baada ya kuteuliwa kama mgombea wa chama cha ODM, nilipelekwa kortini nikajikuta kwamba nimo katika chama cha ANC. Msajili anayesimamia alikuwa amesema mimi ni mwanachama wa ANC na hakuna hata wakati mmoja niliwahi kuwa kule lakini ukiangalia kwenye sajili, zinasema kwamba Mhe. Kizito ni mwanachama wa ANC. Kwa hivyo, niliweza kurudi tena kwa uchaguzi kwa sababu hiyo. Lazima akae ange angaalie rekodi hizo sawasawa ili tusije tukawa na balaa na belua kama hiyo. Kama unavyojua, sisi wanasiasa mara nyingi tunakuwa na mambo yetu ya kisiasa ambayo si ya kanisa bali ya kaisari. Kwa hivyo, sisi lazima tuachiwe njia yetu pia tufanye vile tunavyotaka lakini naye pia awe ange ili tuweze kushirikiana vizuri. Nikirejelea suala la yule bwana aliyebanduliwa nje, ningependa kumuunga mkoni sana Mhe. Dennitah kwamba kweli kijana yule amefanya bidii na ameonyesha kwamba yeye ni shujaa."
}