GET /api/v0.1/hansard/entries/1015762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1015762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1015762/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": "Ningependa kumtolea kongole na nimpatie heko kubwa kabisa kwa kuwa ni swala nzuri kujaribu. Ningependa kumkumbusha kijana yule kuwa ameshinda kwa sababu amefika kiwango cha Rais wa nchi hii. Amri Jeshi Mkuu kuweza kuweka kidole kuwa anafaa lakini wale wahitifadhi wakutarazaki wenye ujuzi akina Otiende, waliingilia pale wakaweza kuona kwamba yeye hatoshi. Tumpee moyo siku nyingine atapata. Nampa kongole kwa sababu amefanya bidii sana. Lakini kwa mujibu wa taharudhi na kanuni zinazosimamia mambo hayo hangeweza kupata fursa hiyo. Nampa kongole. Labda niseme tunastahili tutafute namna ya kuweza kuwapatia nafasi vijana wetu tukiangalia sheria zetu tulegeze mahali fulani kwa sababu ya vijana kwa sababu tukitafuta ujuzi ama tajiriba fulani atakuwa amepata wapi? Labda ni mtu amesoma ametoka tu shuleni lakini sasa tunaangalia ujuzi, tajiriba, miaka mingapi na amesomea nini. Swala hilo huwa linachanganya na linaweza tuweka mahali pabaya sana. Kwa hivyo, ningependa kuomba nchi hii iweze kuwaangalia hawa watu kwa sababu unaweza kumpata mzee wa miaka 50 lakini ana akili kidogo kuliko kijana ama unaweza mpata kijana aliye na akili nyingi kuliko mzee. Kwa hivyo, swala la umri lisiwe kikwazo. Isiwe tu ni tajiriba. Inaweza kuwa ni tajiriba mbaya ya wizi tu. Ujuzi wako mwingi miaka arubaini lakini ni wizi tu."
}