GET /api/v0.1/hansard/entries/1016072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1016072,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016072/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kama kuna eneo ambalo limeonewa tokea Uhuru hadi leo, ni Pwani. Haki za watu wa Lamu zimezoroteshwa. Ninataka kumuunga mkono ndugu yangu mdogo Sen. Loitiptip kwa swala hili. Sisi tunajua watu wanaoishi Lamu ni Waamu na Wabajuni. Lakini ukienda Lamu, utaona mashamba yao yanamilikiwa na watu wengine. Watu hawa wana stakabadhi bandia walizopata kutoka kwa Wizara ya Ardhi. Bw. Spika, ninataka ndugu yangu Sen. Mwangi ambaye ni mkakamavu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kuangalia kwa undani usimamizi wa LKBMU. Tunajua upeo wa baharini ni wa burudani. Lakini utaona upeo ulio katika ziwa la Kenyatta umetolewa stakabadhi na kupewa watu binafsi ambao hawajulikani. Sisi tanawajua watu hawa. Mwenyekiti akileta ripoti yake, mimi nitatoboa na kusema ni akina nani waliopewa ardhi ya watu w Lamu iliyo chini ya LKBMU . Wakati huo ukifika mimi nitasema. Watu wa Lamu ni unyonge kwa sababu ardhi yao ilinyakuliwa."
}