GET /api/v0.1/hansard/entries/1016084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1016084,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016084/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, shukrani. Swala hili linaweza kutatuliwa vizuri kama ile Ripoti ya Ukweli, Haki na Maridhiano itatolewa na kuwekwa wazi kwa wakenya wote. Tunasikia vuguvugu tu, lakini ikitolewa wazi kwa wananchi, nina hakika iko na majina, maeneo ambayo yanachukuliwa kupitia njia ya dhulma. Ninaongea nikijua historia ya Kenya, kwamba mashamba hususan ya Pwani yalichukuliwa kwa njia ya dhulma. Taarifa kama hii Seneta wa Lamu ameuliza ni muhimu kuona ardhi iliyochukuliwa kwa njia ambayo ni kinyume na sheria, kuonewa na kupokonywa, imerudishiwa wenyewe. Hadi leo, watu wanaenda kufukuzwa katika mashamba yao na kuambiwa kwamba, shamba limepeanwa. Shamanba limepeanwa kwa nani ilhali sisi tumeishi hapa zaidi ya miaka hamsini?"
}