GET /api/v0.1/hansard/entries/1016428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1016428,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016428/?format=api",
    "text_counter": 32,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia arifa ya Sen.(Dr.) Mbito kuhusu utalii wa nyumbani. Kutoka janga la korona liingie katika ulimwengu, biashara ya utalii imeathirika pakubwa, hasa hapa nchini. Utalii ni huduma iliyogatuliwa. Ni matarajio yetu kuwa Serikali kuu ingekuja na mwongozo wa kuimarisha utalii nchini. Hata hivyo, kumekuwa na kimya kingi upande wa Serikali. Ni juhudi za wenye biashara za utalii ambazo zimesaidia kufufua utalii katika nchi yetu. Kwa mfano, majuzi kulikuwa na kivutio kikubwa cha utalii kule Watamu wakati kulikuwa na kuhama kwa wale papa wakubwa kuingia Bahari ya Hindi na kuelekea Afrika Kusini. Hii ilikuwa fursa kubwa ya kuwaonyesha Wakenya kwamba utalii una vivutio vyake vingi katika nchi yetu."
}