GET /api/v0.1/hansard/entries/1016429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1016429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016429/?format=api",
"text_counter": 33,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hivi majuzi tulikuwa na kuhama kwa nyumbu kule Maasai Mara. Kuhama huko huwa ni kivutio kikubwa cha watalii hususan wa Kenya. Hata hivyo, Wakenya wengi wameathirika na korona kwa sababu biashara zao zimezama na uchumi kuzorota. Hawana uwezo wa kuzuru sehemu kama hizi ili kujivinjari, kusoma na kuangalia ni vitu gani ambavyo wanaweza kuona katika maeneo yao."
}