GET /api/v0.1/hansard/entries/1016448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1016448,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016448/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Mimi ninataka kuenda sambamba na ile taarifa ya Sen. (Dr.) Mbito. Utalii ni muhimu sana kwa taifa hili. Vijana wengi katika vyuo vya utalii walipendelea sana kusomea utalii kwa sababu ilikua ni biashara kubwa na ilichangia pakubwa nafasi za kazi. Lakini hivi sasa ukiangalia, utaona ya kwamba wamepoteza nafasi hizo. Katika eneo la Pwani, utalii wote umekufa. Utapata watu wameketi katika mitaa kwa sababu hawana la kufanya. Wanaenda kwa mambo ya mjengo na mambo mengine ambayo si ya utalii. Ninaishtumu Serikali kwa sababu jambo lolote kwao linalohusu kuhusu eneo la Pwani ni bahari na starehe kubwa katika mahoteli. Lakini, hawafikirii kuwa kuna vijiji ambavyo nikama maeneo ya Maasai Mara ambapo watalii huenda katika vijiji vya wamaasai kuona jinsi wanavyoishi. Katika maeneo ya Pwani, kuna vijiji kama kule alikozaliwa, kuishi na kufariki Mekatilili wa Menza. Maeneo hayo pia yako wazi kwa utalii. Lakini, Serikali haitii msisitizo wa aina yoyote kuona kwamba maeneo kama lile la Shujaa Mekatilili wa Menza limepewa kipau mbele ili liweze kustawisha utalii katika maeneo hayo. Ukizingatia utalii bila kutengeneza barabara, hutakuwa umefanya jambo lolote. Watu wasifikirie kuwa utalii pekee ndio unafaa kule pwani. Barabara katika vitongoji mbalimbali zinafaa kutengenezwa ili kuwe na mbinu za usafiri kuelekea maeneo ya utalii na burudani."
}