GET /api/v0.1/hansard/entries/1016450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1016450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1016450/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kuna hoteli za Wazungu kama kule Malindi. Maeneo ya utalii yamezoroteka. Watalii wanakuja lakini wengi wanakwenda katika nyumba za watu binafsi. Hiyo inafanya Serikali kukosa ushuru. Wale wanaohusika na utoaji wa kodi za utalii wanafaa kujua kuna mabwenyenye wanaoleta watalii kutoka ng’ambo na kusema ni wageni wao. Wakiwa huko, wanafanya safari zao kisirisiri na kutoka malipo kwa wenyeji wao bila kutoa ushuru ambao unasaidia Serikali kuendeleza mambo ya utalii. Nasisitiza kwamba wasimamizi wa mambo ya utalii wachunguze watu wanaofanya Serikali kutopata ushuru."
}