GET /api/v0.1/hansard/entries/1017161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1017161,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1017161/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii pia kuzungumzia suala hili ambalo ni la kikatiba na ambalo tayari limeweka nchi hii kwenye hali ya wasiwasi. Katiba ya mwaka wa 2010 - Katiba yetu mpya- ilivyokuwa inatengenezwa ilikuwa kwa sababu ya matatizo yale ambayo tulikuwa tumeyapata wakati watu walikosana. Pia vile, wananchi mara nyingi walisema kuwa kwa sababu ya yale makosa yaliyokuwemo ni vizuri kuwa na Katiba mpya. Mheshimiwa Spika, Wakenya wengi walitaka kuwa Katiba mpya ije ili mamlaka mengine yapunguzwe yaende kwenye ugatuzi ili hapa juu tubaki tukiangalia maswala ambayo yanaweza kuendeleza nchi hii mbele wakati ugatuzi nao pia unaendeleza kaunti zetu mbele. Mheshimiwa Spika, nilikuwa Waziri wa Jinsia baada ya Katiba hii kupitishwa mwaka wa 2010, mwezi wa Agosti. Mheshimiwa Spika, swala hili la Kipengele cha 27 (8), limetutatiza mno maanake tayari kiko kwenye ukurasa wa haki zetu na vile ni kuwa huwezi kukigusa kipengele hiki kama hutarudi kwenye kielelezo, yani referendum. Mheshimiwa Spika, jambo linalonisikitisha ni kuwa mtu akipatiwa kazi ya uongozi kuna umuhimu wa huyo mtu kufahamu kuwa Kenya si ya mtu mmoja ama watu wawili bali Kenya ni watu karibu milioni hamsini. Mheshimiwa Spika, Kipengele hiki cha 27 (8) ambacho kinatumika kinahakikisha kwamba Bunge hili la kitaifa halina watu wa jinsia moja, haswa wanawake. Tungependa kuona wanawake wakichaguliwa nchi hii lakini Wakenya wana haki- kama vile mwenzangu alivyotaja, Mheshimiwa Olago Aluoch- kuchagua katika kipengele cha 38. Wana haki ya kuchagua mtu yeyote aliye jinsia ya kike ama ya kiume katika maeneo bunge 290. Mheshimiwa Spika, hatuko hapa kubahatisha. Wakenya waliamua kutuleta hapa na walivyotuleta sisi hawakujua kuwa eti kuna wanawake na wanaume hapa nchini. Mara kwa mara mimi husikia watu wakiuliza ni kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}