GET /api/v0.1/hansard/entries/1017162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1017162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1017162/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nini hatufanani na Rwanda, ama Afrika Kusini. Mheshimiwa Spika, haiwezekani kwa sababu wale wanachaguliwa kupitia orodha ya vyama vya kisiasa. Sisi hapa Kenya kuna tofauti kubwa sana. Kupitia Kipengele cha 38 Wakenya hupiga kura kuamua ni nani atakayewawakilisha hapa Bungeni. Mheshimiwa Spika, nilivokuwa Waziri wa Jinsia, tulijaribu tukaongea na Mheshimiwa Rais akamtuma Mkuu wa Sheria kwenye Mahakama Kuu ili tuweze kupata njia mwafaka vile tutaweza kuongeza idadi ya kina mama hapa nchini. Wakatuelezea kuwa wanatupatia miaka mitano ili tuweze kupata njia mwafaka lakini Mahakama Kuu haikusema kinaga-ubaga swala hili litatatuliwa vipi. Walitaja kuwa swala hili ni lazima lipatiwe muda hadi hapo tutakapofikia idadi ya kina mama jinsi inavyotakikana. Mheshimiwa Spika, mwenzetu Mheshimiwa Otiende Amollo alikuwa na bahati ya kuwa kwenye wale ambao walikuwa wataalam wa kuandika Katiba. Jambo ambalo hawataki kusema wazi ni kuwa waliangalia wakajua kuwa katika Bunge la Kitaifa ukisema utaongezea idadi jinsi wanavyofikiria, haitawezekana. Ndio ukaona kuwa kwenye Kipengele cha 177- kwa ugatuzi, kwenye Bunge za Ugatuzi- waliamua kuweka kipengele ambacho kitaweza kuongezea jinsia hiyo nyingine. Waliiweka bayana na kila mtu akisoma anajua kuwa wanapatikana vipi. Japo kuwa vile ningependa kusema kuwa walivyokiweka kile kipengele kimechezewa. Huwezi kuwa maeneo yetu ya Bunge za Ugatuzi ni 1450 lakini wanaochaguliwa kupitia njia ile wanafika nafikiria Wabunge 800. Mheshimiwa Spika, ukiangalia hesabu tayari inakuchanganya. Bila shaka, Bunge la Senate waliona kuwa walipatie Kipengele cha 98 kinachoeleza akina mama ama wabunge wa jinsia nyingine watapatikana vipi lakini kwenye Bunge la Kitaifa ilishindikana. Mheshimiwa Spika, Kipengele cha 27 (8) kinasema kuwa watu wote ambao ni Wakenya, haswa wale ambao wamepatiwa nafasi za uongozi hapa nchini, na sio Wabunge peke yake, ndio wako na nafasi ya uongozi. Uongozi upo katika mahakama, na hata Ofisi ya Rais kupitia kwa Baraza lake la Mawaziri. Nafasi hizo ziko. Kipengele cha 27 kinataja kuwa sio wenye kuchaguliwa peke yake kwenye Bunge la Kenya ndio lazima wawe thuluthi zisizo pita mbili katika jinsia moja. Inataja hata wale wanaopatiwa kazi upande huo mwingine kwa hiyo mikono miwili ya kiserikali wawe pia wana idadi ya kutosha ambayo haitapita thuluthi mbili. Mheshimiwa Spika, kwa nini liwe Bunge ndilo litabeba kashfa hii ambayo inatakikana kubebwa na Kenya nzima? Inatakikana kubebwa na uongozi wote hapa nchini. Nilikuwa na wasiwasi ya kwamba siku moja tutakuja kuwa na Jaji Mkuu ambaye atafanya vitu bila kuuliza na kuweza kuzungumza na washikadau wote ili kuweza kutatua tatizo hili. Mheshimiwa Spika, Bunge la Kumi na Moja lilijaribu sana. Bunge hili limejaribu kufikiria kuwa sheria hii tutaileta vipi na sio rahisi manake huwezi kulazimisha mtu kupiga kura kwa njia fulani. Halafu isitoshe, hupigi kura tu. Ni lazima tufikirie upigaji wetu kura hapa je unaleta faida gani ama unaleta nini hapa nchini. Kwa mfano, ikiwa tutaongezea Wabunge 80, je watakaa wapi? Huo ndio ukweli wa maneno jamani na mficha uchi hazai! Napenda kusema wazi kuwa hayo yote tumeyafikiria. Ndio ningependa kuona wanawake wanaongezeka. Ningependa tutafute njia ya kuleta akina mama zaidi lakini je, Wakenya wenyewe watatupatia hiyo njia? Tunashukuru kuwa Katiba hiyo imetupatia akina mama 47 kupitia njia ya Wawakilishi wa Kina Mama. Lakini juu ya hapo, tukumbuke hata Bunge la Seneti la Kwanza hakuna mama hata mmoja alikuwa amechaguliwa. Sasa hivi Wakenya wamejaribu wakaleta akina mama watatu. Wakichanganya na wale 20 ambao wako pale unakuta Bunge la Seneti tayari limefikisha idadi inayohitajika. Shida kubwa tuliyoko nayo ni hapa kwenye Bunge la Kitaifa. Nataka kina mama waongezeke lakini je, tutaongeza kupita kinyume na vile wananchi wanavyotaka? Tutaongeza bila kurudi kwa wananchi kuwauliza? Mheshimiwa Spika, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}