GET /api/v0.1/hansard/entries/1017791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1017791,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1017791/?format=api",
"text_counter": 375,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada huu wa ugonjwa wa saratani nchini Kenya. Namshukuru Mhe. Gladys Wanga kwa sababu katika Bunge lililopita la kumi na moja, alikuja na hoja kuhusu saratani katika nchi yetu ya Kenya. Ninamshukuru kwa sababu hivi leo ameleta Mswada katika Bunge hili ndiposa sisi kama Wabunge tupate nafasi kuuchangia. Ugonjwa wa saratani, vile wenzangu wamesema, ni ugonjwa mbaya sana. Katika eneo langu la Trans Nzoia, tumepoteza watu wengi sana kwa saratani. Juzi nilipoteza mpigaji kura wangu mmoja na tukawa na mgonjwa aliyeamka na kusema kwamba jinsi mwenzake alivyopoteza maisha yake, yeye pia ako na ugonjwa wa saratani. Cha kushangaza ni kwamba hatuwezi kupata mashine ya kupima ugonjwa huu katika eneo langu. Inalazimu mgonjwa aje katika hospitali ya Aga Khan. Iwapo huu Mswada utatekelezwa, utaokoa maisha ya watu wengi sana. Huu ugonjwa wa saratani huja na masaibu kadhaa. Mtu anaweza kuwa na ugonjwa wa saratani ya damu, wa koo au wa matiti. Vile wenzangu wamesema, inakuwa vigumu mtu kusema anaugua huu ugonjwa mpaka apimwe. Iwapo hatuna hizo mashine katika sehemu zetu, tunapoteza watu wetu. Nilitembelea hospitali ya Texas Cancer Centre hapa Nairobi. Ukifika hapo, utaona kwamba wewe unayetembea umshukuru Mungu. Wenzetu kule nje wanaumia sana. Nimemsikia Mhe. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}