GET /api/v0.1/hansard/entries/1017792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1017792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1017792/?format=api",
"text_counter": 376,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Caleb akisema tunaweza kuwa na dawa za kienyeji. Naona ni vizuri sana, lakini ni lazima tuwe na mahabara zetu za kupima madawa hayo. Wengi wanaotumia madawa ya kienyeji wanasema huenda yanaponya ugonjwa wa ukimwi, wengine wanasema inawapatia nguvu. Tukiwa na mahabara ambazo zinaweza kupima hayo madawa na yasaidie watu, itakuwa nzuri. Iwapo hatujafunza hawa watu jinsi ya kutumia hizi mashine au iwapo hawajapata ujumbe kamili, hiyo ni changamoto. Nimewasikia wenzangu pia wakisema huu ugonjwa utangazwe kuwa janga la kitaifa katika nchi yetu ya Kenya. Hiyo ni sawa. Lakini tusipotekeleza haya, hayatakuwa na manufaa na hayatasaidia wagonjwa ambao wameathirika na huu ugonjwa wa saratani. Wacha Mswada huu utekelezwe jinsi tunavyosema kama viongozi. Hilo litakuwa jambo zuri. Ninamshukuru tena Mhe. Wanga kwa kuleta Mswada huu katika Bunge hili ndiposa sisi pia kama Wabunge tuujadili. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi."
}