GET /api/v0.1/hansard/entries/1018199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1018199,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1018199/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, KMC ni shirika ambalo kwa muda mrefu limefanya bishara na kuhudumia wakenya. Katika Kaunti ya Mombasa tulikuwa na depot kubwa ambamo kulikuwa na wanyama kutoka Somalia wakisafirishwa kwenda masoko ya nje. Kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, hatujaona shughuli yoyote ikiendelea katika KMC, Mombasa. Bw. Spika, swala la kuipeleka KMC kwa Wizara ya Ulinzi ni jambo ambalo linafaa kukemewa. Jambo hili limefanywa kinyume na sheria. KMC ni shirika lililoundwa kisheria; kulikuwa na mswada wa kisheria uliopitishwa ili kuunda KMC. Haiwezi chukuliwa kienyenji na kupelekwa katika Wizara ya Ulinzi bila taarifa yoyote ya kisheria. Bw. Spika, tunajua ya kwamba kazi ya Jeshi kubwa ni ulinzi wa Kitaifa. Wanalinda mipaka yetu. Kufanya biashara sio moja ya kazi ambazo wanajeshi wanafaa kufanya. Swala hili lazima lichunguzwe kwa undani na Kamati. Kutoka mwaka huu uanze tumeona mashirika kadhaa yakitolewa katika mahali pake na kupelekwa sehemu zingine bila kufuata sheria. Bw. Spika, Taarifa hii imekuja wakati mwafaka. Jana tulizungumzia maswala ya"
}