GET /api/v0.1/hansard/entries/1018218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1018218,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1018218/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana baba yangu kwa kunipatia wasia huo. Uliyoyasema ni kweli kabisa. Tangu utotoni tunajua kwamba wale ambao hubeba bunduki ni askari ili kutulinda sisi. Tukiona waliova nguo za kijani kibichi, tunajua ni wanajeshi wetu ambao hulinda mipaka yetu na kuhakikisha usalama wa nchi. Ninashukuru sana kwamba katika maeneo ambayo baba yangu, Sen. Haji, ameweza kutembea, ameona maswala kama hayo yakiendelea. Lakini hapa Kenya, ni mara ya kwanza kihistoria kuona wanajeshi wakihusika na mambo ya kuuza ng’ombe. Hata Wakenya wenyewe watashangaa sana wakiwaona wanajeshi wakiuza ng’ombe. Tabia kama hii tumeona hivi majuzi. Wale walio katika vyuo vya kijeshi wanapewa makazi ya utawala. Utawala ni tofauti na kuwa mkubwa wa majeshi. Ukirudi kwa barabara na kuanza kutawala, ule utamu utauhisi, ni mtamu sana. Tukiendelea hivi, wanajeshi watajiunga na siasa na kwingineko. Hatima ya mambo haya, watakuja kujitwalia mamlaka kimabavu. Si vizuri tuwakubalie kusimamia KMC na kuuza nyama kwa nchi nyingine na kuhesabu ng’ombe na mbuzi ni wangapi ni jambo tunalipinga kwa sabau halifai. Huo mkataba pia ni makosa na kinyume cha Sheria, kwa sababu, hakuna wananchi wowote walioulizwa, katika uhusishwaji wa uma: “Je, nyinyi kama Wakenya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}