GET /api/v0.1/hansard/entries/1018249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1018249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1018249/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Ni vizuri kuwa Sen. Haji ameongea kinagaubaga leo na kusema kuwa Waziri wa Wizara ya Interior & Coordination of National Government aweze kuja mbele ya Seneti hii. Pia mimi kule Tana River County nasumbuliwa na watu ambao vijana wao wamekosekana katika hali ya sintofahamu. Bw. Spika, kuna mandugu wawili waliouwawa kinyama katika sehemu ya Mnazini. Waliuwawa usiku na watu waliojitambulisha kama polisi. Mpaka siku ya leo, sisi hatujui kama hao watu walikua polisi au walikua majambazi. Kwa hivyo, ni hali ya kutatanisha sana na tumekua katika hali ya hofu. Nikienda sehemu ya Mombasa kuna watu ambao wamekosekana mpaka leo na hawajulikani mahali walipo. Kule Pwani tuko katika hali tatanishi na vijana wako katika hali ya tahadhari kubwa sana. Hii taarifa ambayo imetolewa na Sen. (Dr.) Ali ni ya kweli na sisi tungetaka hao Waziri wawili waje mbele ya Seneti hii watueleze mahali watu wetu wako. Asante Sana."
}