GET /api/v0.1/hansard/entries/1018901/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1018901,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1018901/?format=api",
    "text_counter": 754,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Ninawapongeza Team Kenya kwa umoja wetu na kwa kazi nzuri ambayo tulifanya kuhakikisha kwamba tumeleta usawa katika ugavi wa rasilmali. Umoja wetu ndiyo ulikuwa nguvu yetu na sote tulisimama pamoja kidete kuhakikisha hakuna kaunti ambayo inapoteza pesa zozote. Pili, ninapongeza Kamati ya Maseneta kumi na wawili ambao walikaa pamoja tena baada ya kushindwa kupata muafaka kwa muda wa mikutano 19, lakini wamekaa pamoja wakapata muafaka. Ndiyo maana leo kila mtu anayetoka ana furaha. Hata wengine wanaweza kwenda kulala na viatu bila kuvivua. Sisi ni Maseneta wa Jamhuri ya Kenya, wala sio Meseneta wa kaunti zetu. Ninawakosoa wale walikuwa na hofu kwamba mimi nikifika kwetu nitaweza kupoteza kura kwa sababu nimepiga kura na wale ambao walikuwa wanapoteza wakati kaunti yangu inapata. Kwa sababu hiyo, ninawapongeza wale ndugu zangu saba ambao walisimama na sisi Team Kenya. Kwa kuwa nia yetu ilikuwa safi na ya Kenya, hata wale walikuwa na hofu kwamba kaunti zao zitapoteza wamepata. Tukiangalia, kwa mfano, Sen. Cherargei wa Kaunti ya Nandi, ameweza kupata zaidi ya zile ambazo alikuwa apate awali. Umoja wetu ndio umetuleta hapa ambapo tumefika. Kama Seneti, lazima tuweze kuhakikisha kwamba umoja huu unaendelea kutekelezwa. Kaunti kama vile Mombasa, ilikuwa inapoteza zaidi ya Kshs800 milioni, lakini kwa ushupavu wetu, tumeweza kuhakikisha kwamba, wameongezewa Kshs500 milioni zaidi. Mapato yetu sasa ni Kshs1.3 bilioni, katika Mwaka wa Kifedha 2021/2022. Mhe. Bi. Spika wa Muda, mapambano yanaendelea kwa sababu tatizo lililoko ni kuwa, lazima tuondoe suala la ugavi wa rasilmali kutoka kwa Wizara ya Fedha na Mipango na iletwe hapa Bunge. Hapa ndipo pahali maalum ambapo Katiba inasema pesa zigawanywe. Hatuwezi kuwa tukienda na bakuli kwa Wizara ya Fedha na Mipango kila mara kuomba na Idara ya Mahakama inakwenda pale pia kuomba. Hayo yote ni kinyume cha Katiba yetu. Kutekeleza Katiba kamili, ni lazima tuondoe vitengo vyote vya Serikali katika minyororo ya Serikali kuu ili kuhakikisha kwamba, kaunti zetu zinastawi."
}