GET /api/v0.1/hansard/entries/1018991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1018991,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1018991/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, upande wa pwani tungependa kuona wale wanaotambuliwa kama Mekatilili wa Menza, aliyepigania Uhuru wakati ule. Imekuwa utovu wa nidhani katika Serikali, kwamba hawawezi kutambuliwa baada ya kufariki miaka mingi iliyopita. Alikuwa mama wa kwanza katika upiganiaji wa Uhuru, aliyepiga Mzungu kofi na akafungwa. Alifungwa katika jela ya Kisii lakini kwa ujasiri wake alitoka na kutembea kwa miguu mpaka akarudi nyumbani, Kilifi. Watu kama hawa hatuwezi kuwasahau katika historia ya nchi yetu. Mama kama Mepoho alikuwa mpiganiaji mkubwa wa Uhuru. Mwaka jana, tulipoteza bibi ya aliyekuwa kiongozi wa Pwani wa kisheria wa hali ya juu sana; bibi wa Ronald Gideon Ngala. Watu kama hawa wasipoteze hadhi ya Wakenya. Wasifiwe, maanake, waliacha nguzo na mienendo ya kufurahisha na kusaidia watu wa jami yao na Wakenya wote."
}