GET /api/v0.1/hansard/entries/1019131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1019131,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019131/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Wetangula. Kuku alivishwa kilemba, watu wakamuona kama jogoo, lakini kuku ni kuku, na jogoo ni jogoo. Kwa muda wa wiki moja sasa, tumeona Mwenyekiti wa Baraza la Magavana akitoa taarifa ambazo hazina msingi kikatiba na kisheria. Kwanza, alisema kuwa atavunja Bunge la Seneti. Bunge la Seneti liko katika Katiba. Asome Articles 93 hadi 96 na kuendelea, aone majukumu ya Seneti ni nini, ili aone kuwa Bunge la Seneti liko hapa kikatiba na haliwezi kuondolewa mpaka Katiba ibadilishwe kupitia referendum. Leo ametoa barua. Wiki iliopita alitoa vitisho kuwa atasimamisha huduma katika kaunti zetu. Tumeangalia sheria zote zinazohusu kaunti zetu, na hakuna mahali ambapo Mwenyekiti wa Baraza la Magavana ana amri ya kusema kwamba huduma zisitishwe. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}