GET /api/v0.1/hansard/entries/1019132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1019132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019132/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Hana mamlaka kabisa kuhusiana na utendakazi wa kaunti zingine. Yeye ana mamlaka chache katika kaunti yake. Bi. Spika wa Muda, ni kejeli kubwa Gavana Oparanya kusema kwamba atazuia huduma za afya. Ametaja mahali ambapo panamuathiri yule mwananchi wa chini kabisa. Hivi sasa, tuko katikati ya Janga la Corona (COVID-19). Wananchi wanapata shida kupata huduma za afya ilhali yeye anasema kwamba huduma za afya zisitishwe katika kaunti zetu. Hii sio dharau kwa Wakenya pekee, ila pia kwa Rais wetu. Jana, katika mkutano ambao uliongozwa na Rais Kenyatta, Gavana Oparanya, viongozi wa Bunge la Seneti na Kiranja wetu, Sen. Kwamboka, walikuwa pale. Sen. Kwamboka alikua ameshikilia fimbo yake ya Kiranja. Kwa hivyo, hii ni madharau kwa Bunge la Seneti na kwa taifa kwa sababu Gavana Oparanya hana mamlaka ya kuzuia huduma katika kaunti yoyote. Natoa onyo kwa magavana wote 46. Gavana Oparanya anaweza kusitisha huduma katika Kaunti ya Kakamega, lakini zile kaunti zingine 46 wapuuze amri yake, kwa sababu amri ile haina mamlaka yoyote ya kisheri ambayo inaweza kusaidia kuwatetea wakati kitakapoumana. Asante kwa kunipa fursa hii."
}