GET /api/v0.1/hansard/entries/1019167/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1019167,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019167/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyoletwa hapa na Sen. Wetangula. Kuna msemo was Kiswahili unaosema, “Afadhali kuungua kidole kuliko kuunguwa mdomo.” Mdomo uliotumiwa na Gavana Oparanya sio mdomo mzuri katika nchi yetu ya Kenya. Gavana yule anajua kwamba Seneti inapigana kuhakikisha kwamba pesa zinagawanywa katika kaunti zote sawa. Hapo jana, Gavana Oparanya alikuwa katika mkutano na Rais Uhuru Kenya, Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga na viongozi wengine wa Seneti kuzungumzia jambo la ugavi wa fedha kwa kanti zote 47. Nilifurahi kusikia kwamba Rais Kenyatta aliahidi kuongeza zaidi ya Kshs50 bilioni. Nilishangaa sana kusikia Gavana Oparanya akiaamuru zahanati na hospitali katika kaunti zote 47 kufungwa. Kitendo alichokifanya Gavana Oparanya ni cha aibu na ninakilaani. Gavana huyo asijaribu kuamuru hospitali katika kaunti zote kufungwa. Hivi majuzi, kamati ya COVID- 19 ilikuja Kwale kuzuru hali hospitali katika kaunti hiyo wakati huu wa COVID-19. Niliandamana na Kamati inayozingatia maswala ya COVID-19 na nikazungumza na Gavana wa Kaunti ya Kwale. Nilimueleza Gavana wa Kaunti ya Kwale kwamba asidanganywe na Gavana Oparanya kufunga hospitali zote katika Kaunti ya Kwale. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}