GET /api/v0.1/hansard/entries/1019168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1019168,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019168/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Naunga Sen. Wetangula mkono kwamba Mungu akipenda, kesho kutaonekana moshi hapa Seneti tutakapo afikiana katika mambo ya ugavi wa fedha kwa na kaunti zote kupata pesa. Ninalaani kitendo cha Gavana Oparanya. Nikisikia kwamba hospitali yoye imefungwa kesho katika kaunti yoyote, tutamchukulia gavana husika sheria kali sana. Sisi kama maseneta, tunapigania haki za kaunti zetu zote 47 hivyo Gavana Oparanya hana haki ya kuamuru hospitali yoyoye kufungwa. Ningependa kumkumbusha ndugu yangu Gavana Oparanya kwamba ‘Afadhali kuungua kidole kuliko kuunguwa mdomo.’ Huo mdomo uliozungumza unafaa kuomba msamaha. Asante sana Bi. Spika wa Muda."
}