GET /api/v0.1/hansard/entries/1019183/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1019183,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019183/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Arifa ambayo imetolewa na Seneta wa Bungoma. Kwa kweli, vile rafiki yangu Seneta wa Mombasa alivyosema, kichwa cha kuku hakistahili kilemba. Ndipo unapoona hakika gavana huyu wa Kakamega anachukuwa hatamu za county zote za Kenya akisema ya kwamba, anatishia ya kwamba atapeleka watu katika likizo za lazima. Pia zahanati zote na mahospitali zifungwe. Hana habari ya kwamba Wakenya wengi maskini wanagharamikia pesa zao kwenda kupata matibabu katika hospitali hizi. Yeye akikaa huko Kakamega, akiwa na shida zake tele za Kakamega, anatupa hizo shida katika nchi nzima ya Kenya, kuenda kwenye Baraza la Magavana na kusema ya kwamba atapeleka watu likizo, watu waende likizo ya lazima na pia hospitali zifungwe. Pia, alirusha mawe kwa upande wa Bunge la Seneti; Bunge hili ambalo limejaa watu ambao akili zao ni timamu, waheshimiwa ambao wanajua dunia inatoka wapi na inaelekea wapi. Yeye anasema atafunga Seneti na kujiletea hali ambayo yeye yuko nayo katika saa hii. Saa hii unavyoona, Seneta wote katika Seneti hii walichangamka, wakakasirika na kusema “wewe unatupa mawe katika Seneti hii ambayo iko na watu wa kisawa sawa, watu ambao akili zao ni mzuri.” Na wewe sijui umetumia nini huko Kakamega, unaamka asubuhi, unasema utapeleka watu waende likizo, utafunga hospitali zote; kisha Bunge la Senate pia halifai, wewe utaenda kufunga bunge hiyo. Basi mimi ninakuambia ya kwamba shida yako ya Kakamega, wacha ikuwe shida yako ya Kakamega. Usituletee shida zako za Kakamega katika county zile zingine ambazo tuko na usalama na tunaendeleza mambo yetu kwa njia ya utaratibu kabisa. Na pia ningependa kutoa wito kwa gavana wangu. Wewe ni gavana ambaye tumekuchagua Tana River. Kama utaenda kusikiza shida za Kakamega, uende kufunga hospitali moja, uende kupeleka watu likizo, basi sisi tutateremka na wewe. Kwa sababu shida ya Kakamega ni shida ya Kakamega na shida ya Tana River, ni ya Tana River. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}