GET /api/v0.1/hansard/entries/1019214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1019214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019214/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Mimi pia ninaunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Faki. Kenya Ports Authority (KPA) imekua tegemeo kubwa kwa watu wa Pwani lakini tukichukua Usimamizi wa Bandari na kuichanganya na Shirika la Reli na Shirika linalohusika na bomba la kusafirisha mafuta, ni ukiukaji wa sheria. Ni jambo la kusikitisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Kenya anaendelea kugandamiza watu wa Pwani, hususan kiuchumi. Watu wametegemea sana Usimamizi wa Bandari. Ukienda Mombasa leo, utapata kwamba watu wengi ni hohehahe kama mayatima. Hukana uchumi wa aina yoyote unaongeza mapato kwa wananchi wa Mombasa unaoendelea. Si wafanyibiashara wala akina mama wanaouza vitu vyao asubuhi kwa watu wanaoenda kazi katika Bandari. Si watu wa kupata vibarua pale ndani wala madereva na wanaobeba mizigo. Kila kitu ni kama kimechukuliwa. Tunavyoongea ni kama bandari imeondolewa. Hata wale akina mama ambao baada ya kazi wanaume wangeweza kuji--- Unaelewa. Ni makosa sana kuwa uchumi umeharibika kwa sababu ya amri kama hii. Hii amri imekiuka sheria za Kenya na Katiba ambayo ni kuu kuliko sheria zote. Hii inamaanisha kwamba Rais alikosea kisheria alipotoa hii amri bila kufanya majadiliano na wananchi wanaoishi katika eneo hilo. Hata Katiba inasema “ there shall beconsultation.” Ni lazima ahusishe wale wanaoishi pale kwa kuwaambia: “Ninataka kufanya hivi na vile. Je, mnaonaje?” Anafaa kupata maoni na mwawaidha, lakini hakukuwa na majadiliano ya aina yotote. Sikuona gavana akiulizwa: “Hii bandari tunataka kuitoa hapa tuipeleke Naivasha.” Sikuona gavana akiitwa na kuulizwa maoni yake na ya wananchi wakiunganisha na Kenya Railways Corporation na Kenya Pipeline. Hayo yaliofanywa ni ukiukaji wa sheria na Katiba ya Kenya. Mimi ninamuenzi sana Rais. Yeye ni mtu ambaye hana makosa kwa sababu yeye akipelekewa makaratasi na kuulizwa: “Je, umeone kuwa hii ni sawa?” Kisha akatia sahihi yake. Sasa inaonekana kuwa Mkuu wa Sheria wa Jamhuri wa Kenya ameshindwa na anazembea kazini. Hili ni jambo la aibu kwa sababu alikua hakimu kama mimi. Ninasikitika sana kwa sababu angeenda kwa Rais na kumwambia: “Kabla hujaidhinisha hatua kama hii, ni kinyume cha sheria.” Alikosea na hakuenda. Jambo la pili ambalo ni kosa kubwa ni kwamba---"
}