GET /api/v0.1/hansard/entries/1020225/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1020225,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1020225/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": {
        "id": 13287,
        "legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
        "slug": "kassim-sawa-tandaza"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu wa maana ambao ikiwa utatekelezwa, utaweza kuokoa maisha ya watu wengi katika nchi hili. Ni jambo la kuhuzunisha sana unapoangalia takwimu za watalaam wa ugonjwa wa kansa kama ilivyotajwa awali. Wataalamu ni takriban arobaini nchi nzima kati ya watu takriban millioni hamsini. Takwimu zinasema twapoteza watu elfu thelathini kila mwaka. Hizi ni takwimu zinazotoka kwa wale amabao walipata fursa ya kuenda hospitalini na ikajulikana kitaalamu kuwa wanaugua kansa. Ninavyojua ni kwamba wengi wanaougua ugonjwa huu huwa wanafariki bila kwenda hospitali kwa sababu ya gharama ya kwenda hospitali na ya kuchunguzwa. Mara nyingi, wagonjwa wa kansa huwa inasemekana kuwa hutolewa kipande cha nyama sehemu ambazo ugonjwa upo. Ikiwa ni mgonjwa ambaye anatoka, kwa mfano, sehemu ninakotoka za Kwale kama Shimba Hills, Lungalunga ama Tiribe, mtu huyu kufika mahali ambapo anatolewa kile kipande cha nyama ndio kiweze kuletwa Nairobi ndio kufanyiwa huo utafiti baadaye kisha arudi apate majibu yale kwa yule daktari. Mara nyingi huwa wengi wanavunjika moyo na wanaacha kufuatilia. Hatimaye labda atapatiwa tu madawa ya kupunguza maumivu na kusema labda ni Mwenyezi Mungu ndiye amepanga hali hiyo. Kwa hivyo, Mswada huu utahakikisha kwamba kuna wataalam wa kutosha. Pili, si lazima kuwe na huo utaalam wa kwamba ile zahanati atakayoenda mgonjwa kuwe na utaratibu wa kuona ni vipi atafikiwa mtaalam huyu mahali pale alipo bila kugharamika mtu kusafiri, aidha kuenda hosipitali kuu, kama Coast General Hospital kule kwetu, na hatimaye kuja Nairobi katika Kenyatta National Hospital, ambayo gharama yake hawa hawawezi kupata ule usaidizi na kujulikana ni saratani ya aina gani na inahitaji matibabu aina gani. Lakini si hapo pekee, kwa sababu hata ikiwa ataambiwa kweli ni saratani na matibabu ni haya, gharama ya matibabu bado iko ghali na mtu yule bado hatasaidika. Upande mwingine, kwa wale wataalamu ambao tunasema wapatiwe mafunzo, tatizo kubwa ambalo tunalijua ni kwamba hatimaye hawawezi kutoa huduma hizi kwa sababu ya vile wanavyochukuliwa. Saa hizi kuna sehemu zingine katika nchi hii ambazo madaktari na wauguzi wa kawaida wanagoma kwa sababu ya kukosa mishahara. Kwa hivyo, ikiwa tutaweza kufundisha hawa wataalamu wa saratani, pia lazima serikali kuu na zile za kaunti wawalipe vilivyo ili wafanye kazi zao. Haisadii mtu kuwa na utaalamu lakini asiweze kuutumia kwa sababu aidha hana vifaa ama yeye mwenyewe hapati marupuru yanayomtosheleza. Asante sana kwa hayo niliyoyanena. Naunga mkono Mswada huu na ushughulikiwe vilivyo."
}