GET /api/v0.1/hansard/entries/1020534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1020534,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1020534/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuchangia Ripoti iliyoletwa na Mhe. Sheriff Nassir. Kwanza, nina bahati kuwa nilisoma na Sheriff Nassir darasa moja. Nimebahatika kuwa naye Bunge kwa mara ya pili. Naielewa kazi yake na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, anatosha kuwa Gavana wa Mombasa. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ukaguzi wa hesabu ni jambo ambalo kama Wabunge lazima tulizingatie kwa makini. Kulingana na sheria ya Kenya, yeyote ambaye ana haki ya shamba lolote sharti awe na hati miliki. Tukiangalia mtiririko wa Ripoti hii, ni wazi kuwa mashirika mengi ya Serikali hayana hati miliki. Kama Kamati ya Mashamba, tumepokea migogoro mingi baina ya wananchi na mashirika ya Serikali. Tumeweza kutatua migogoro hiyo kwa kuita Wizara ya Mashamba na kuipa kauli mbiu kuwa kuna haja ya kuzunguka na kuhakikisha kuwa mashirika ya Serikali yamepata hati miliki. Kama ilivyosemwa, kama Wabunge tunajinyima nguvu. Tuna nguvu za kikatiba kuwa kila ripoti inayopitishwa hapa sharti itekelezwa na wahusika. Kwa sababu hatuna mipango msingi, ripoti nyingi zikipitishwa na Bunge hili zinapatikana kwenye meza za wahusika. Ukiangalia Equalisation Fund ambayo imekuwa ikitolewa kwa sababu ya kuleta usawa, ukiangalia sehemu ninayowakilisha, pesa za Serikali zimetumika kuchimba visima sita. Visima vimesimama kwa sababu aliyekuwa kiongozi wa shirika la maji, aliondoka na mwingine kuletwa. Aliyeingia ameshindwa kukamilisha pale ambapo pesa za umma zimetumika. Ukamilishaji wa miradi ni muhimu na kama Wabunge, tuna nguvu nyingi kama wawakilishi wa wananchi. Tukiwa hapa kama Wabunge 290 sharti tuangalie masuala yanayowahusu wananchi. Kauli mbiu kutoka Bunge hili sharti ipewe uzito. Bila kuweka uzito, tutaendelea kuleta ripoti nyingi. Tumeleta ripoti nyingi kuhusu mashamba yanayochukuliwa na mashirika mbalimbali kiholelaholela na Wabunge wengine wameleta masuala ya mashamba kuhusu wananchi wao kupelekwa mbio. Tunapitisha ripoti hizo lakini hazipatiwi uzito. Kwa yale ambayo yamepitishwa katika Ripoti hii na Mhe. Sheriff Nassir na Kamati yake ni kuwa yafuatiliwe, yaangiliwe na yakamilishwe. Hata ile Kamati ya Utekelezaji haina nguvu nyingi. Ni ukweli kuwa imepatiwa nguvu lakini hazikamilishi masuala kama haya. Katiba inasema wazi kuwa kama Wabunge tuna nguvu ya kufanya shauri na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}