GET /api/v0.1/hansard/entries/1020824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1020824,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1020824/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Tumeshukuru kupata habari kuwa Bw. Yassin ameachiliwa. Kuachiliwa kwake hakuturidhishi kwa sababu tunataka kufahamu sababu ya kushikwa na kuwekwa ndani muda huo wote. Tuliona kwenye runinga jinsi familia yake ilivyoteseka na jinsi afya yake ilidhoofika kupitia mateso aliyoyapata. Ni Lazima tufuatilie zaidi tujue sababu ya kukamatwa na ikiwa alipata matatizo, apate fidia. Inawezekana kuna Wakenya wengine ambao wanashikwa ovyo ovyo bila sababu. Iwapo tutafuatilia kwa kina, wataweza kuachiliwa bila kushtakiwa. Ninaamini kuwa tukifuatilia kujua tatizo na sababu za kuachiliwa kwake, tunaweza kusimamisha mambo kama haya."
}