GET /api/v0.1/hansard/entries/1020942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1020942,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1020942/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": "Mhe. Gladys amesema kunafaa kuwa na mafunzo ya ugonjwa wa Saratani. Huu ni ukweli, kwa sababu watu wengi husafiri kutoka kule mashinani na wanaenda nchi za nje kutafuta matibabu, ilhali tuko na watafiti wa kutosha katika taifa hili. Kitu ambacho kimekosa ni mafunzo kuhusu huu ugonjwa wa Saratani na wale ambao wanafaa kuwa wanashinikiza yale matibabu katika zile hospitali zetu katika kaunti. Wakati ambapo haya mafunzo yataidhinishwa na kusisitizwa yawe yakifanyika hapa na watafiti wengi wafunzwe, watu wengi katika taifa hili watajua hali zao za afya. Wakati mwingine, mtu hugundua ya kwamba ako na Saratani akiwa katika kiwango cha mwisho. Hili jambo hufanya familia nyingi kutumia hela nyingi maanake wanagundua ugonjwa katika dakika ya mwisho. Wakati ambapo haya matibabu yatakuwa yanaangaziwa wakati mgonjwa anaenda hospitalini na pia huu ugonjwa utakuwa wa kwanza kuangaliwa, watu wengi watapona kwa sababu watakuwa wanajua hali zao mapema pale hospitalini. Hospitali zingine zina vifaa vya kutosha lakini hakuna wataalam wakuzitumia kwa sababu hawajapewa mafunzo ya kuwawezesha kutumia zile mashine zinazotumika kufanya utafifiti wa ugonjwa huu."
}