GET /api/v0.1/hansard/entries/1021066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1021066,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1021066/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamwad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika. Historia inajirejelea. Nakumbuka kauli ambayo wenzangu wameitaja ya kuwa Umma haukuhusishwa katika jambo hili licha ya kuwa ni sharti kikatiba. Hili ni Jumba ambalo linaenda na mambo yaliyotangulia kabla yetu. Miaka takriban miwili iliyopita nilipoinuka katika Jumba hili na kuzungumza ya kuwa mambo ya privatisation ya bandari ya Mombasa hayakuhusisha watu, baadhi ya watu walisema yale yale ambayo ndugu yangu Mhe. T.J. Kajwang’ anaambiwa – ya kuwa ana watu ambao anawasaidia. Wengine wameambiwa lugha hiyo kwa sababu ya kuzungumza sauti ile ya Wakenya iliyosababisha sheria ile ile kukataliwa. Kwa sababu haikufuatwa kisawasawa, ilienda nje na mahakama ikaamua kuwa sio sawa. Sasa hili Bunge lisiwe la kutumika kutengeneza sheria na baadaye kuonekana kuwa zile sheria zilijaribu kupitishwa kimabavu. Kwa hivyo namsihi mwenzangu sana. Ni kwa sababu ya mambo ambayo tutazorota na hapa hapa katika Jumba hili. Kando na haya ambayo ni mambo ya National Aviation Bill, kuna mengine ambayo yatakuja hapa. Yanahusiana na mkataba wa kuunganisha Kenya Ports Authority, Kenya Railways, Kenya Pipeline na pia ICDC. Hayajakuja hapa lakini yatakuja. Yakifika hapa tutayazungumza na vile vile wenzetu walivyoambiwa kuwa wana yale wanataka, tutawazungumza hapa hapa katika Jumba hili hili. Mhe. Spika, ningependa kuwasihi wenzangu kuwa tufuate mamlaka ambayo tumepewa, sio tu kuzungumza kule nje lakini kupitia Jumba hili, tuwatetee watu wetu. Kila mmoja wetu ameapishwa kikatiba kwa kushika kitabu cha dini yake ili kuhakikisha kuwa mambo ya Wakenya waliotuchagua yatakuwa ya kwanza."
}