GET /api/v0.1/hansard/entries/1021605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1021605,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1021605/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Taita Taveta CWR), JP): Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia swala hili ambalo ni muhimu kabisa, na nampongeza Mhe. Swarup Mishra kwa kuleta swala hili wakati sawa kabisa. Tunajua ni kweli, Mhe. Naibu Spika wa Muda, ya kwamba Wakenya wengi sana wanasafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta matibabu. Ni wakati sasa, karne hii, hata hapa nchini Kenya, tuweze kubadilisha hilo. Tunajua linawezekana kwa sababu hili suala la matibabu ya nje ya nchi limekuwa kama biashara sasa. Wakenya wanatumwa kutibiwa nje mwa nchi mara kwa mara na wakati mwingine, haijalishi kama wana uwezo ama hawana. Hilo limetubidi kupata matatizo ya kuwa kwa michango mara nyingi sana kwa ajili ya kuwafanyia michango, ilhali maswala mengine ni yale ambayo yanaweza kutibiwa humu humu nchini. Tumeona vyema, wakati huu wa janga hili la Coronavirus, ya kwamba watu wengi ambao walipaswa kwenda nchi za nje kutibiwa hawakuweza kwenda na wengine wao walitibiwa humu humu nchini na wakapata afueni. Kwa hivyo, inaonekana kuwa mengine yanaweza kufanyika humu nchini. Naunga mkono Mswada huu. Ni vyema kuwa sasa tuwe na mwongozo dhabiti kama nchi zingine ambazo zinatusaidia kwa masuala haya ya matibabu, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}