GET /api/v0.1/hansard/entries/1022682/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1022682,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1022682/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Mwanzo kabisa, naunga mkono Kamati ya Ardhi maanake nimesoma Ripoti yake kwa uangalifu na undani kabisa. Kwa ukweli, hata mpita njia akisoma hii Ripoti, ataona kabisa kuna ulaghai mwingi sana ambao ulikuwa umeendelea, lakini Kamati ya Ardhi imefanya kazi nzuri. Watu wa Eneo Bunge la Roysambu wanaumizwa tu. Ukiangalia kwa sura, utaona ya kwamba yule mzungu, Bwana Samuels, aliyefariki, alikuwa anaendelea na shughuli vizuri kabisa na wananchi wa kule Roysambu. Alikuwa anawalipa vizuri lakini kwa bahati mbaya, alifariki. Alitoa maagizo kwamba waendelee kukaa pale na wajaribu kujizatiti angalau wapate mlo wa siku. Baada ya wale ndugu zake kurejea, kwa bahati mbaya, walifurushwa. Sijui ni nani alifanya hivyo. Kwa ukweli, hata wale watu ambao wako kule ndani na shule wapatiwe title deeds zao."
}