GET /api/v0.1/hansard/entries/1023698/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1023698,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1023698/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
    "speaker": {
        "id": 13379,
        "legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
        "slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika. Ningependa kumpongeza Mwenyekiti mpya wa Kamati ya NG-CDF. Ninamwombea heri katika kazi yake. Kitu ambacho ningependa kusisitiza ni kwamba kuna Maeneo Bunge maskini ambayo yanategemea huu mgao wa NG-CDF. Kusema kweli, hivi sasa watu wengi wanateseka. Hawaoni maendeleo. Wamezoea kuona kazi nzuri inayofanywa na NG-CDF. Pia, ningependa kuomba hizi pesa zitolewe mara moja. Sio kwamba tusubiri ama tuambiwe leo ama keshokutwa. Wananchi wanateseka na wanaomba miradi ifike mashinani mara moja. Pia, yapo Maeneo Bunge mengine ambayo mpaka sasa Kamati zake hazijapitishwa hapo bungeni. Imekuwa miezi mingi na hatujui sababu ni nini. Kwa hivyo, ningependa kuomba majina hayo yaongezwe kwenye mjadala huu unaouzungumzia mgao wa NG-CDF."
}