GET /api/v0.1/hansard/entries/1024294/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1024294,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024294/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "wataweza kuipitisha Ripoti hii ya kurasa 600. Nina imani ya kuwa tangu tulipoileta hii Ripoti na kuipeleka katika Bunge, Wajumbe wameweza kuisoma. Leo kuna jambo muhimu. Naongea kama Mkenya mmoja ambaye alichaguliwa na maelfu ya wanamvita. Naongea kwa niaba ya wenzangu 18 ambao wamechaguliwa na wenzao katika maeneo yao. Bunge hili likiweza kupitisha Ripoti hii, nina imani ya kuwa sauti ya Kenya itakuwa imewika. Kamati imefanya kazi yake. Naomba, kwa unyenyekevu, sekta zote za Serikali, kwasababu...Ndani ya Ripoti hii tumetaja watu ambao ni lazima Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) iwafungulie mashtaka. Tumetaja watu ambao hawastahili kushikilia nyadhifa katika mashirika tofauti tofauti ya Serikali. Tumezungumza hapa na kutaja ya kuwa baadhi ya mashirika yachunguzwe, wakiwemo watu ambao wanafaa kwenda mbele ya mahakama. Tumetoa amri kwa Directorate of Criminal Investigations (DCI) wahakikishe ya kuwa wale wamepora mali ya umma waende mbele ya mahakama wakajitetee huko. Hii ni kwa sababu Kenya tunayotaka ni ile haina hali yoyote ya ufisadi. Hii Ripoti pia imeweka wazi yakuwa licha yakuwa kila Mbunge anatoka chama tofauti, mimi kama Mwenyekiti wao nikiwa ni wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) hakuna hata siku moja mmoja wetu hapa alipigiwa na kinara wa chama chake nakuambiwa yakuwa lazima…"
}