GET /api/v0.1/hansard/entries/1024296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1024296,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024296/?format=api",
    "text_counter": 386,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamwad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Bila shaka, kama Mbunge mkongwe. Nilikuwa nasema tu yakuwa Kamati iliendeshwa bila msukosuko wowote wa kisiasa. Nataka tu kuzungumza kwa uchache kwa sababu nataka wenzangu wazungumze natukamilishe ili iwe sheria leo. Leo hii tukiweza kumaliza, iwe sheria. Mashirika ambayo tumeweka katika Ripoti hii ni 48. Naisihi National Land Commission (NLC), kamisheni ambayo iliwekwa katika Katiba, kuhakikisha kwamba mambo ya ardhi yametatuliwa kisawasawa. Itoe title deed kwa haya mashirika ya Serikali hususa yale ambayo yamenyakuliwa na mabepari. Ardhi lazima irejeshwe ili iwafae Wakenya wote. Pia kuna mashirika ambayo yalikuwa yanateta bila kuelewana yanadaiana. Tumetoa amri kwayo kuwa badala ya watu kupelekana kortini na kulumbana, ni lazima head of public service, ambaye ni mkuu wao, awakalishe chini ili ajaribu kutatua hili jambo bila ya kupoteza fedha. Hilo ni jambo ambalo linahuzunisha Wakenya wengi. Kuhusu ununuzi, nawasihi wenzangu wakubali kupitisha hii Ripoti. Hivyo, waliofanya ufisadi wa aina yoyote kwa mambo ya procurement katika mashirika haya 48 wachukuliwe hatua za kisheria ili hii Kenya ijue yakuwa Bunge lina meno yakuuma. Limeuma na halitaweza kuwacha suala la vita dhidi ya haya mambo yaliyoko ya corruption. Kuna mambo mengine tumekataa. Wenzangu watakubaliana na mimi. Siwezi kuletewa Ripoti kisha ukiangalia ile Ripoti baadaye unaambiwa ya kuwa mashirika fulani kama Kenya Power (KP), Kenya Electricity Generating Company (KenGen), Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) yakuhusika na barabara, Kenya Rural Roads Authority (KURA), kwa muda wa miaka sita au saba, hayajaweza kukosa hata jambo lolote moja. Tukiangalia katika vyombo vya habari na kusoma magazeti, unaona wazi ya kuwa ufisadi umekithiri ndani ya mashirika haya. Kwa hivyo, tumetoa amri kama Ripoti iliyopita. Tunasema katika Ripoti hii kuwa kwa yale mashirika ambayo tunayashuku na tumepata fununu zozote, ni lazima tupate internal audit zao. Aidha tupatiwe ripoti yenye kuhusika na management response na management letters. Hivyo, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}