GET /api/v0.1/hansard/entries/1024297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024297,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024297/?format=api",
"text_counter": 387,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamwad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "tutaweza kutoa uamuzi, kama Kamati, iwapo ni kweli vyombo vya habari vimezua au kulikuwa na ukweli fulani katika masuala yale. Nikimalizia, kuna jambo lingine ambalo mashirika yanaweza kuchezea. Ni hili jambo la riba, interest. Unapeana kandarasi kwa mtu, unaamua kutomlipa yule mtu kwa muda unaofaa. Ndani ya hii Ripoti kuna wale ambao tuna waambia “Ikiwa watu watadai riba kwa njia yoyote, ni lazima Board of Directors na management wapelekwe mbele na kusema ni kwa nini wanalipa riba.” Ukisoma hii Ripoti, mabilioni ya pesa, sio mamilioni, ambayo yangeweza Kulipa madeni ya nchi hii yanalipwa kwa wanakandarasi kwa sababu ya riba. Kisa na sababu? Kuna mmoja anaamua yakuwa hataki kulipa ili watu wale rushwa ile riba ikiongezwa. Mwishowe, tumezungumza hili katika Ripoti iliyopita ya 22 na Rais akakubali. Tunamsihi tena kuwa yale mashirika ambayo Board of Directors na wale Managing Directors, ikiwa kuna wale ambao hawajapewa nafasi zile muafaka wateuliwe ili tusiwe na watu walioko katika mamlaka na hawajui hatima yao iko vipi. Nina imani kuwa wale walioko hapa wataliunga jambo hili na Ripoti hii mkono. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Namuomba ndugu yangu, Naibu Mwenyekiti, Abdi anikubalie katika jambo hili."
}