GET /api/v0.1/hansard/entries/1024558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024558/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tayari nchi ilikua imegawanyika kati ya walahai and walahoi. Zile kaunti 19 ambazo zilikua zinapoteza pesa walikua wanajiita walalahoi na wale 28 ambao walikua wanapata walikua wanajiita walalahai. Hiyo ingekua ni kugawanya nchi yetu ambayo waanzilishi walitoa damu, rasilimali zao na maisha yao ili kuahakikisha tuko na Kenya moja. Tunapoimba wimbo wa taifa, tunasema haki iwe ngao na mlinzi. Haki hii ni ipi? Tunapozungumzia haki, je ni sawa kaunti 19 zipoteze pesa kwa sababu tunapata zingine 28 ambazo zinaongezewa? Hiyo siyo haki ambayo tunazungumzia katika wimbo wetu wa taifa, kwamba haki iwe ngao na mlinzi. Pendekezo la kuaihirisha mjadala litatoa fursa Maseneta wakae chini pamoja wazungumzie swala hili bila kuleta mgawanyiko katika nchi ama vyama. Hii ni kwa sababu tunaona vyama vilikua na hatari ya kupasuka. Chama chetu cha ODM, Maseneta saba walipiga kura juzi kupinga Hoja ya Sen. Kang’ata na wengine watano wakapiga kuunga mkono. Hiyo ni dhahiri kwamba tayari vyama vilikua vinapata misukosuko na hiyo inge maanisha kwamba tunapoenda mbele wakati tunajadiliana maswala ya Building BridgesInitiative (BBI) ingekua nchi ambayo inapelekwa katika njia isiyokua sawa. Nampongeza Sen. Murkomen aliyekuwa Kiongozi wa Wengi hapo awali kwa kuja na Hoja hii ya kuaihirisha mjadala kwa sababu inatoa fursa kwa Bunge la Seneti kuangalia swala hili tena kwa undani zaidi ili tuhakikishe haki inatendeka kwa wananchi wote wa Kenya. Kama Maseneta na kaunti zao, tunaunganika katika kiuno. Hatuwezi sema kaunti fulani haifai ama ingine haina idadi kubwa ya wananchi. Kaunti zote zina tegemeana. Kwa hivyo, lazima Hoja itakayoletwa izingatie nchi nzima kwa jumla. Bw. Spika, wakati tulipozungumzia swala hili wiki iliyopita, sote tuliona kwamba kuna haja ya Maseneta kukaa chini na kuangalia usawa unapatikana katika nchi yetu. Tusijipige kifua kuwa sisi ni wengi ama sisi tunapata, la. Wakati unapoangalia, angalia kama maswala ya Kenya iko mbele ama maswala ya nyumbani kwetu yako sawa. Tukieka maswala ya Kenya mbele, tutaona kwamba kuna haja ya Maseneta na watu kukaa chini na kuhakikisha kwamba haki inatendewa kwa WaKenya wote. Bw. Spika, kama Seneta wa Mombasa, ninaunga mkono Hoja ya kuaihirisha mjadala ili tutoe fursa kwa watu kuangalia swala hili kwa makini na kuhakikisha kuwa Kenya inabakia moja na wananchi wote wanapata haki. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Hoja ya Sen. Murkomen"
}