GET /api/v0.1/hansard/entries/1024706/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024706,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024706/?format=api",
"text_counter": 364,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Saa 2.30 p.m. tulipokuwa tunaingia hapa, askari walikuwa wamejaa hapa nje wakiangalia sisi ilhali kama hiyo haikubaliwi katika Bunge. Pia Sen. Malalah amepata tishio kama hilo. Tutaendelea hivi kwa miaka mingapi? Hii ni kwa sababu katika historia ya Bunge la Kenya, tunajua kwamba ukishakisiwa kuwa wewe ni mtu wa msimamo fulani, basi unaweza kupatikana katika msitu wa Ngong.Wabunge waliokuwa wakakamavu katika siasa walipoteza maisha yao ndani ya msitu wa Ngong. Hatutaki kuona msemo kama huo ukisemwa ama ukitokea hivi sasa. Sen. Sakaja ni kijana mdogo sana ambaye ana familia changa. Sitaki kuamka kesho asubuhi na kusoma kwamba yeye amepoteza maisha yake huko Ngong Forest. Tunamhitaji hapa Nairobi. Ni kijana ambaye amejitolea muhanga, kufa kupona, kuona kwamba Kenya ni nchi moja. Sote tuko hapa kwa sababu ya ugavi wa pesa zinazokwenda katika serikali za mashinani. Uongozi wa upande wa walio wengi ukiongozwa na Sen. Poghisio umefeli mtihani; hawawezi hiyo kazi. Sisemi kitu ambacho hakiko sawa. Sen. Kang’ata hawezi kumshawishi hata Seneta mmoja upande wake wa walio wengi kuenda upande wowote. Kuna umuhimu kwamba tuwe kitu kimoja ili Kenya ibaki kuwa nchi moja. Asante, Bi. Naibu Spika."
}