GET /api/v0.1/hansard/entries/1024833/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024833,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024833/?format=api",
"text_counter": 491,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza ningependa kumpongeza Salim Mwidadi na wenzake kwa kuleta malalamiko haya katika Seneti. Hii inamaanisha kwamba wana imani kwamba watapata haki katika hii Seneti. Jambo la pili ni kuwa hii ni baadhi ya dhuluma za kihistoria ambazo zilitokea katika Jamhuri ya Kenya. Kama walivyosema katika malalamiko yao, mmishonari Ludwig Krapf alipoingia Kenya, alisafiri mpaka Rabai ambako alianzisha kanisa yake ya kwanza. Wakati huo, watu walisafiri kwa miguu. Wakati huo walikuwa wanatumia Old Port. Mtu alipofika hapo, alilazimishwa kutumia dau au vihori kusafiri mpaka Jomvu Kuu kisha aanze safari kwa miguu kuelekea sehemu zingine. Wakati huo, Jomvu Kuu ilikuwa mwanzo wa safari zote kuelekea bara. Krapf hakujenga kanisa Jomvu Kuu kwa sababu wengi wa wakazi wake walikuwa Waislamu. Kwa hivyo, aliingia ndani na kuanzisha kanisa yake katika maeneo ya Rabai."
}