GET /api/v0.1/hansard/entries/1024838/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1024838,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024838/?format=api",
    "text_counter": 496,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "(NLC) ilipoanzishwa, walipata fursa ya kuangalia swala hili lakini hakuna chochote kiliweza kufanyika. Ndio maana wakaazi wakaja katika Bunge la Seneti kutaka wapewe haki kwamba ardhi hii ni yao ya kihistoria. Ni ardhi ambayo wameikalia zaidi ya miaka 100 sasa kutoka walipoanza kukaa mahali pale. Wameiutumia kwa ukulima, kuenda baharini kuvua na kama sehemu yao ya kale ya kuweza kuomba Mungu wakati wanahitajika. Tunaomba kamati husika iangalie swala hili kwa undani na haraka. Juzi, wiki mbili zilizopita, kulifanyika maandamano makubwa katika eneo la Jomvu kuu ambapo baadhi ya watu waliweza kushikwa na polisi kwa sababu wameandamana kutaka haki yao."
}