GET /api/v0.1/hansard/entries/1024840/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024840,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024840/?format=api",
"text_counter": 498,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, Katiba yetu inatoa fursa kwa watu kuandamana wakati kuna matatizo au wakati wanataka kueleza malalamiko yao. Hatuoni sababu gani watu wale waliweza kukamatwa na kupelekwa mahakamani wakati kitu walikuwa wanatetea ni ya haki yao ya kuweza kupewa ardhi yao ya kihistoria. Ardhi ndiyo chombo kikubwa cha uzalishaji mali. Hatuwezi kuwanyima wakaazi wa Jomvu ardhi yao kwa sababu ya dhulma za kihistoria ambazo zimefanyika katika nchi yetu hii. Katiba yetu ya 2010 inarejesha haki kama hizi kwa wenyeji ili waweze kupata haki zao na kuona kwamba haki inatendeka katika eneo lile. Bi Naibu Spika, ninaunga mkono malalamiko haya ya watu wa Jomvu. Tunataka kamati husika ifuatilie swala hili kwa haraka ili tuweze kupata ufafanuzi mapema kabla hakujatokea maafa kutokana na swala hili. Asante."
}